
Watoto wawili mjini Babati mkoani Manyara mmoja mwenye umri wa miaka 14 na mwingine mwenye umri wa miaka 7 (Majina yamehifadhiwa) wamemwagiwa maji ya moto na mama yao mzazi hali iliyopelekea watoto wale kuungua miili yao hadi ngozi kubanduka.
Tukio hili limetokea siku ya Jumapili iliyopita ambapo inasemekana kuwa msamaria mwema ambaye ni jirani wa familia hiyo aliamua kuliibua jambo hili kwa kutoa taarifa katika ofisi ya ustawi wa Jamii mjini humo.
Akiongea na mwandishi wetu, Christina ambaye ni afisa ustawi wa Jamii mjini hapo amesema tarehe 24, Agosti mwaka huu asubuhi walipokea watoto hao wawili kutoka kwa wasamaria wema wakiwa wameongozana na baba yao mzazi wakiwa wamemwagiwa maji ya moto na mama yao.
Watoto walisema chanzo cha tukio hilo ni kuwa kulikuwa na maji yalikuwa yametengwa jikoni kwa ajili ya ugali ndipo mama aliwataka wabadilishe sufuria hiyo waweke nyingine. Wakati yule mtoto mkubwa akiwa anabadilisha ile sufuria, kile kitendo cha kubadilisha maji na kuyaweka kwenye sufuria nyingine kwa bahati mbaya yale maji yakamdondokea mama yao mguuni ndipo mama akajawa hasira akaamua kuyachukua yale maji na kumwagia yule mtoto mkubwa. Kitendo cha kummwagia maji yale yule mtoto, mtoto mdogo pia akawa anakatisha pembeni ya yule mtoto mkubwa hivyo yale maji yakawamwagikia watoto wote wawili
Baba yao mzazi Peter Costantine alieleza kuwa siku ya Jumapili yeye alikuwa kijiweni ambapo mke wake alikuja akaomba hela kwa kwa ajili ya mboga mida ya saa 12:30 jioni.
"Baada ya nusu saa nilirejea nyumbani na nilipokaribia nyumbani nikaona watu wamejaa na kubaini kuwa watoto walikuwa wanalia, nilipouliza kwa wale watu wakasema sisi tumesikia watoto wanalia ndipo tukaamua kuja kuona nini kinaendelea" Alisema baba wa watoto hao.
Baba mzazi anasema alipoingia ndani alikuta watoto wanalia na aipowauliza wakasema wamemwagiwa maji na mama yao.