
Kisubi amejiunga na Polisi Tanzania akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Simba ambao walimsajili kwa miaka mitatu akitokea Tanzania Prisons.
Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Robert Munisi, alisema ni kweli wamemalizana na kipa huyo akiwa huru wanatarajia mazuri kutoka kwake kutokana na uzoefu mkubwa alionao kwenye ligi.
"Ujio wake utakuwa na tija kwenye kikosi chetu baada ya kuondoka kwa Metacha tulikuwa na Kelvin Igendelezi ambaye hana uzoefu mkubwa ujio wa Kisubi utaongeza chachu ya ushindani," alisema Munisi na kuongeza;
"Tunahitaji kuwa na kikosi bora na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kwenye kila nafasi uwepo wake utatoa changamoto kwa aliyemkuta na tunaamini ataongeza kitu kwenye timu yetu.
Wakati huohuo Kisubi alisema yeye ni mali ya Polisi Tanzania kwa sasa baada ya makubaliano ya pande mbili kati yake na Simba kuhusu kuvunja mkataba kukamilika.
"Ni kweli nilikuwa na mkataba wa miaka mitatu na Simba ambao walinitoa kwa mkopo Mtibwa Sugar baada ya kumaliza mkataba wa mkopo nimekaa mezani na uongozi wa Simba na kukubaliana kuvunja mkataba ili niwe huru baada ya hilo kukamilika ndipo nilipoamua kumalizana na Polisi Tanzania nimejifunga huko miaka miwili." alisema.
Tags:
michezo