HAMISA MOBETTO AFUNGUKA SABABU YA DIAMOND KUTOKUMPOST MWANAYE SIKU YA KUZALIWA KWAKE



MWANAMITINDO Hamisa Mobetto amejibu sababu za kwa nini mzazi mwenzake Nassib Abdul ambaye ni msanii wa bongo fleva kutompost mtoto wao Dylan siku ya kuzaliwa kwake.

Mwanamitindo huyo kupitia mahojiano na chombo kimoja cha Habari nchini aliulizwa kwa nini mzazi mwenzake Diamond Platnumz hakumpost mtoto wao siku ya kuzaliwa kwake ambayo ilikuwa siku ya Agosti 8 mwaka huu, mwanamitindo huyo amesema kuwa hajui sababu ya Diamond kutompost mtoto wao.

Aliongeza kwa kusema kuwa labda hilo swali aulizwe baba wa mtoto (Diamond Platnumz) kwa nini hajampost mtoto wake katika siku ya sikukuu ya kuzaliwa kwake pia akasema kuwa baba yake mwenyewe hakuwahi kuwa na Akaunti ya Instagram hivyo hata yeye hakuwahi kupostiwa na haikuongezea wala kumpunguzia chochote.

Pia aliulizwa kama bado Diamond anatoa matunzo kwa mtoto wao lakini Mobetto hakutaka kuweka wazi suala hilo, ikumbukwe kuwa tu baada ya Diamond kutoshare kwa namna yoyote ile birthday ya mtoto wake siku ya Agosti 8, mwaka huu Hamisa Mobetto alimfuta kwenye Bio ya Instagram katika page ya Dylan.

Post a Comment

Previous Post Next Post