KARANI WA SENSA AJIFUNGUA USIKU WA KUAMKIA SIKU YA SENSA, MTOTO AHESABIWA


Karani wa Sensa ya Watu na Makazi wilayani Bunda mkoa wa Mara amejifungua muda mfupi kabla ya kuanza kazi hiyo, hivyo kulazimika kuondolewa kwenye orodha ya makarani katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari amesema kuwa karani huyo alijifungua usiku wa kuamkia Agosti 23, 2022 ingawa hakuweza kumtaja jina.

"Tangu tumeanza tumepata changamoto ambayo pia ni baraka kuna karani wetu amejifungua usiku na bahati nzuri alijifungua kabla ya saa sita kwahiyo yeye na mtoto wake pia wamehesabiwa na baada ya hali hiyo kujitokeza tayari karani wa akiba ameshachukua nafasi na kazi inaendelea," amesema Nassari.

Chanzo - mwananchi.co.tz

Post a Comment

Previous Post Next Post