SIMBA WAFIKIA MAKUBALIANO BINAFSI NA KELETSO MAKGALWA, MAZUNGUMZO NA SEKHUKHUNE UNITED YAENDELEA


Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano binafsi (personal terms) na winga wa kushoto wa Sekhukhune United ya Afrika Kusini, Keletso Makgalwa (29), ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kukamilisha usajili wake.

Taarifa zinaeleza kuwa pande hizo mbili tayari zimekubaliana kuhusu vipengele vyote vya mkataba, ikiwemo mshahara, bonasi, ada ya kusaini (sign-on fee) pamoja na muda wa mkataba. Inaelezwa pia kuwa kocha Steve Barker amehusika kwa kiasi kikubwa katika mchakato wa kumpendekeza na kumshawishi nyota huyo.

Hata hivyo, usajili huo bado haujakamilika rasmi, kwani mazungumzo kati ya Simba SC na Sekhukhune United kuhusu ada ya uhamisho yanaendelea. Endapo klabu hizo zitafikia mwafaka, basi Makgalwa anatarajiwa kutua Msimbazi rasmi.

Wakati huo huo, wapinzani wao wa jadi, Yanga SC, nao wanaendelea na mazungumzo na Sekhukhune United kuhusu mchezaji huyo, jambo linaloifanya vita ya kuwania saini yake kuendelea kuwa ya ushindani mkubwa.

Post a Comment

0 Comments