Aliyekuwa beki wa klabu za Simba SC na TRA United, Chamou Karaboue (26), amekamilisha rasmi uhamisho wake kwenda kujiunga na klabu ya Talaba FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Iraq.

Taarifa zinaeleza kuwa kila kitu kimekamilika baada ya Karaboue kusaini mkataba wa miaka miwili, hatua inayomfungulia ukurasa mpya katika maisha yake ya soka nje ya Tanzania.

Katika klabu hiyo mpya, Karaboue atakuwa mchezaji mwenza wa nyota wa Tanzania, Simon Msuva, jambo linaloongeza idadi ya Watanzania wanaoendelea kuipeperusha bendera ya nchi katika ligi za kimataifa.

Uhamisho huo unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Talaba FC huku ukimpa Karaboue nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika soka la Mashariki ya Kati.