FLYING HORSE YAFUNGUA OFISI ARUSHA, BONDIA EMMANUEL SHIJA AWAHIMIZA WATANZANIA KUCHAGUA UBORA

Kampuni ya ALC Lubricants, wazalishaji na wasambazaji wa vilainishi vya magari kupitia chapa ya Flying Horse, imefungua rasmi ofisi yake ya kwanza ya Kanda ya Kaskazini katika Jiji la Arusha, hatua inayotarajiwa kurahisisha upatikanaji wa bidhaa zake kwa wateja wa Arusha, Kilimanjaro na mikoa mingine ya ukanda huo.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Balozi wa Flying Horse, Emmanuel Shija, ambaye ni Bingwa wa Dunia wa WBC MuayThai katika mchezo wa ngumi na mateke. Shija, akiwa pamoja na timu ya Flying Horse Kanda ya Kaskazini, aliwataka Watanzania kuendelea kuunga mkono bidhaa zenye ubora zinazozalishwa na kusambazwa nchini kwa manufaa ya uchumi na maendeleo ya viwanda.

Akizungumza katika hafla hiyo, Shija amesema Flying Horse imejijengea sifa kwa kutoa vilainishi vinavyozingatia ubora, vinavyolinda injini za magari na mashine huku vikisaidia kupunguza gharama za matengenezo.
"Nimeamua kuwa sehemu ya familia ya Flying Horse kwa sababu naamini katika ubora wa bidhaa zake. Tunataka Watanzania watumie bidhaa zinazowapa thamani halisi ya fedha zao na zinazolinda vyombo vyao vya usafiri na kazi," amesema Shija.

Kufunguliwa kwa ofisi ya Arusha ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma karibu na wateja na kuhakikisha bidhaa za Flying Horse zinapatikana kwa urahisi bila kutegemea usafirishaji kutoka Dar es Salaam.

Flying Horse imejikita katika kuzalisha vilainishi vinavyokidhi mazingira ya Afrika yenye joto kali, mizigo mizito na matumizi ya muda mrefu, huku ikitoa suluhisho kwa sekta za usafiri, madini, viwanda na biashara.

Mbali na mafuta ya injini za magari ya abiria na malori, Flying Horse pia huzalisha na kusambaza bidhaa mbalimbali za vilainishi zinazokidhi mahitaji ya sekta tofauti.

Bidhaa hizo ni pamoja na mafuta ya injini za pikipiki (4T), mafuta ya injini za dizeli aina ya Synthetic CK-4 na CH-4, mafuta ya injini za magari ya petroli yenye kiwango cha API SN, mafuta ya Hydraulic, Gear Oils, vilainishi vya viwandani (Industrial Lubricants), grisi (Greases), mafuta ya breki aina ya Brake Fluid DOT 4, pamoja na vilainishi maalumu vya mashine zinazotumika viwandani na kwenye shughuli za migodini.
Bidhaa hizi zimetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora ili kuongeza ufanisi wa injini na mashine, kupunguza uchakavu wa vifaa na kusaidia watumiaji kupunguza gharama za matengenezo.

Bidhaa hizi pia zimeundwa kuongeza ufanisi wa injini, kupunguza uchakavu wa vifaa, kuongeza muda wa kubadilisha oil na kusaidia wateja kupunguza gharama za uendeshaji.

ALC Lubricants imeendelea kupanua uwepo wake katika Afrika Mashariki na Kati kupitia chapa ya Flying Horse, huku ikisisitiza misingi ya ubora, uaminifu na utendaji bora katika bidhaa zake. Kampuni hiyo pia imeweka wazi kuwa inaendelea kutafuta wasambazaji zaidi ili kuwafikia wateja wengi nchini.



Post a Comment

0 Comments