
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema leo June 27, 2026, majira ya saa 01:00 usiku, kumetokea hitilafu ya kiufundi katika Mfumo wa Gridi ya umeme ya Taifa, hali iliyosababisha mikoa yote inayopata huduma ya umeme kupitia Gridi ya Taifa kukosa huduma hiyo.
TANESCO imesema Wataalamu wa Shirika hilo wanandelea na jitihada za kurejesha huduma ya umeme kwa awamu katika maeneo yaliyoathirika.
“Shirika linawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa usumbufu uliojitokeza na linawashukuru kwa uvumilivu wao wakati jitihada za kurejesha huduma zikiendelea”
0 Comments