WASIRA AFUNGUA OFISI ZA CCM CHIBE SHINYANGA, ATAKA OFISI ZITUMIKE KUTATUA KESRO ZA WANANCHI



MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema ofisi za Chama nchi nzima zinapaswa kutumika kutatua changamoto za wananchi.

Wasira ameyasema hayo leo Machi 26, 2025 alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi za CCM katika Kata ya Chibe, Wialaya na Mkoa wa Shinyanga ambapo ametaka ofisi za Chama ziwe kimbilio la wananchi kufikisha kero zao.

"Nakupongezeni sana kwa kupata ofisi nzuri naomba muitumie kuwasikiliza wananchi wa hapa, kuwasikuliza wanachama wetu, na kufanya vikao ambavyo ajenda zake zinashughulikia mambo ya watu sio kusulihisha magomvi.

"Tuzungumze mambo ya watu, tushughulike, 'miniti' zetu zote zihusu mambo ya watu, yatokanayo tuulizane tulikubaliana machinga wana matatizo haya, je walipatiwa ufumbuzi, tumezungumza wakulima wana matatizo haya je matatizo yao yametatuliwa makundi mbalimbali na wananchi tuwafanye wajue kwamba CCM ndio kimbilio lao," amesisitiza.


Post a Comment

0 Comments