
KOCHA Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi amesema kuwa anaamini nyota Jonathan Ikangalombo atafanya kazi kubwa ndani ya timu hiyo kutokana na uwezo alionao kwenye mechi ambazo anapata nafasi.
Ikangalombo alipata nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida Black Stars ambao ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Uwanja wa Airtel.
Katika mchezo huo uliochezwa Machi 24 2025 walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 huku Ikangalombo akiandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye mchezo wa ushindani.
Miloud amesema kuwa mshambuliaji huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapenda kufunga na kushirikiana na wachezaji wengine katika kutafuta ushindi ndani ya uwanja.
“Ambacho ninakiona kwa Ikangalombo ni uwezo wake hasa kwenye matumizi ya nafasi pamoja na kuwa mwenye spidi ndani ya uwanja hilo linaonekana kutokana na kazi ambayo anafanya hivyo nina amini kwamba kuna mazuri yanakuja.”
0 Comments