
BEKI wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids yupo nje kwenye mipango ya timu hiyo inayojiandaa kuwakabili Waarabu wa Misri, Al Masry katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali.
Che Malone alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Azam FC wababe hao walipogawana pointi mojamoja.
Mchezo huo ulichezwa Februari 24 2025 ambapo mbali na Che Malone kipa namba moja wa Simba, Mousa Camara naye alipata maumivu kwenye mchezo huo.
Ni Aprili 2 Simba wanatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Al Masry ugenini na mchezo mwingine unatarajiwa kuchezwa Aprili 9 2025 ambapo Simba watakuwa nyumbani.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa bado beki Che Malone hajatengamaa hivyo watamkosa kwenye mchezo dhidi ya Al Masry, ugenini.
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kukwea pipa alfajiri ya Machi 28 kuelekea Misri kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa kimataifa.
0 Comments