VIBANDA VYA WAMACHINGA VYATEKETEA KWA MOTO SINGIDA

VIBANDA zaidi ya 50 vya Wafanyabiashara wadogo (Machinga) vilivyopo karibu na Ofisi za Posta Mkoani Singida vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 4, 2022.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Eng. Paskasi Muragili, ambapo amesema chanzo cha moto huo ni kuwa kuna kijana alikuwa anafanya welding (kuchomelea) kwenye kibanda chake na bahati mbaya ukatokea moto kwenye kibanda kimoja cha mwanzoni na baadaye moto ukashika vibanda vyote.
"Hili ni eneo maalum ambalo tulilitenga kwa ajili ya wamachinga, kulikuwa na biashara ya nguo, viatu, Mamalishe n.k kulikuwa na vibanda zaidi ya 100 na vibanda zaidi ya 50 vimeteketea vyote"
"Maeneo haya kuna mnara wa simu, na ofisi nyingine lakini hakuna majengo au miundombinu iliyoathirika, tulikuwa tunahofia jirani kulikuwa na matenki ya mafuta lakini hayajaathirika, kiujumla hakuna Mtu aliyeathirika lakini mali yote katika vibanda hivi zaidi ya 50 imeteketea” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: