KUELEKEA MECHI YA KESHO, MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA WAPIGWA MKWARA MZITO

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans watapapatuana na Simba SC katika mchezo huo ambao utatumika kama kiashirio cha ufunguzi wa Msimu Mpya 2022/23.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne Muliro amezungumza na Waandishi wa Habari na kusema, shabiki yoyote hataruhusiwa kwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa akiwa na silaha isipokuwa vyombo vya dola.
“Katika kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo, usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu”
“Ni marufuku kwa Mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, tunawatoa hofu Mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa kwa kiwango cha juu” amesema Kamanda Muriro
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: