KAULI YA KOCHA NABI KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA SIMBA

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake liko tayari kwa ajili ya mchezo wangu ya jamii dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumamosi katika uuwanjawa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika mkutano maalum na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo Nabi amesema anafahamu ukubwa wa mchezo huo hivyo wamefanya maandalizi mazuri yanayowapa matumaini ya kuibuka na ushindi.

"Ninajua umuhimu wa mchezo huu tumejiandaa vyema. Morali ya wachezaji iko juu, nimependa utayari wao na inanipa matumaini ya kupata matokeo mazuri tutajitolea kwa uwezo wetu tushinde" Alisema Nabi

Nabi amebainisha kuwa wachezaji wako tayari kwa mchezo huo isipokuwa mshambuliaji Lazarus Kambole ambaye alipata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc.

Nabalalisema winga Jesus Moloko atakuwa sehemu ya kikosi siku ya kesho baada ya kupona majeraha ambayo nae aliyapata katika mechi ya Namubgo Fc.

"Moloko (Jesus) na kambole waliumia mechi ya kirafiki dhidi ya Namungo Fc, Moloko yuko tayari kurejea kikosini lakini Kambole bado. Pia tuna wachezaji wapenzi ambao wako tayari na unaweza kunitumia siku ya kesho kagawa wapo wengine tutaendelea kuwaingiza kikosini taratibu."

Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto amewataka mashabiki wa TIMU hiyo kujitokeza kwa wingi dimba la Mkapa kuwapa sapoti wakiwa na dhamira ya kutetea Ngao ya Jamii waliyoshinda msimu uliopita

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.