AZIRAI BAADA YA KUGUNDUA KUWA MKEWE NI MMILIKI WA NYUMBA WALIYOPANGA
Mwanaume mmoja raia wa
Zambia aliyetambulika kwa jina la Martin Stampa, anadaiwa kuanguka na
kuzirai baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye “mwenye nyumba” wake.
Kulingana
na taarifa za mitandao ya kijamii nchini humo, imesema, Stampa (37),
aliishi katika nyumba hiyo kwa miaka 15, na alikuwa akilipa kwacha 3500
kila mwezi ambazo mkewe alidai kuzipeleka kwa mwenye nyumba wao.
Hata
hivyo, inadaiwa kuwa ugomvi ulizuka baada ya bibi huyo aliyetambulika
kwa jina la Lombo Lushomo (27), kugundua kuwa mumewe alikuwa na uhusiano
wa kimapenzi nje ya ndoa.
Martin Stampa, ambaye inasemekana alizirai baada ya kugundua mmiliki wa nyumba aliyopanga ni mkewe. (picha na Within Nigeria/News Pick)
Mitandao hiyo, inaarifu kuwa Martin Stampa alimwambia mke wake kuwa alipata kimada kwa sababu alitaka mtu mwenye akili na anayejihusisha na mazungumzo mahiri ikiwemo kujituma katika utafutaji.
Inadaiwa kuwa, jambo hilo lilimkasirisha Bi. Lushomo, ambaye alimtaka kuhama na kumpisha na kumwambia kuwa hana akili za kutosha kwani amekuwa akimlipa kodi ya kila mwezi kwa sababu nyumba wanayoishi ni yake.
Mara baada ya kuoneshwa hati, ya nyumba hiyo, inasemekana Martin alipoteza fahamu na kuzimia kitu ambacho kilisababisha Wananchi kumpa msaada wa kumwagia maji ili kumzindua kisha kumuwahisha Hospitalini.
No comments: