RAIS SAMIA APONGEZA JUHUDI ZA KUKWAMUA WASICHANA KIELIMU

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) kwa kutazama changamoto ya ufaulu kwa watoto wa kike katika visiwa vya Zanzibar na kuja na suluhu ya kutaka kumaliza tatizo hilo.

Hiyo ni baada ya takwimu kuonyesha ufaulu hafifu kwa watoto wakike visiwani Zanzibar hali inayokwamisha maendeleo ya haraka kwa mtoto wa kike na jamii nzima kwa ujumla

Rais Samia ameyasema hayo leo Juni 19 wakati akizindua Taasisi hiyo uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

“Jambo linalofanya na wenzetu wa MIF ni jambo la kizalendo, linalopaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwani sote tunafahamu kuwa ukimwezesha mwanamke umeiwezesha jamii nzima hivyo taasisi hii inakwenda kuikomboa jamii nzima kupitia juhudi ambazo inafanya kwa mtoto wa kike,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kufunguliwa kwa taasisi hiyo ni jambo moja lakini kutatua changamoto zilizopo ni jambo lingine, hivyo ameipongeza MIF kwa kuonyesha nia ya dhati.

Ofisa Mtendaji Mkuu MIF, Fatma Mwassa amesema kama taasisi, itajihusisha na ukombozi wamwanamke kupitia uwezeshaji kielimu na afya na hata sekta ya kilimo.

“MIF kupitia mpango mkakati wake wa miaka mitano inakusudia kuwa na kituo kitakachoshughulika na watu wenye changamoto za afya ya akili na ulemavu wa kiakili, eneo ambalo mara nyingi husahaulika na nguvu nyingi kuwekezwakwa watu wenye ulemavu wa viungo tu,” anasema Fatma.

Pamoja na kuzinduliwa kwake, taasisi ya MIF tayari imefanikiwa kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi bora wawili wasichana ambao watasomeshwa mpaka pale watakapofika kikomo cha elimu yao.

“Sambamba na hilo MIF imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 10 walioshika nafasi 10 za juu kupata masomo nje ya nchi (Scholarship) kwa wasichana.

“Mpaka sasa MIF imefanikiwa kuwapeleka wanafunzi zaidi ya 100 katika vyuo vya ufundi Tanzania Bara, lakini pia inakusudia kujenga vyoo 150 katikashule mbalimbali nchini ambavyo kati ya hivyo 75 vitajengwaTanzania Bara.”

Taasisi hiyo pia inafanya kazi na wadau wengine mbalimbali ili kutimiza malengo yake na kupitia urabishi wake na mabenki na taasisi nyingine binafsi, pia imeweza kukusanya Sh1.7 bilioni ambazo zitaelekezwa kwenye uendeshaji wa taasisi.

“Vilevile taasisi ya MIF imeingia mkataba na nchi ya falme zakiarabu (U.A.E) ambao hawa watatoa ufadhili wa takribani Sh15 bilioni utakaokwenda kusaidia ujenzi wa kituo cha mafunzo cha Amali-VTC, kituo ambacho kitakwenda kutoa mafunzo yaamali kwa wahitimu 1,000 kila mwaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti na Mwanzilishi wa MIF, Wanu Hafidh Ameir amesema taasisi hiyo itakwenda kutoa msaada kwa jamii bila kujali uwepo wake binafsi ambapo lengo la taasisi hiyo ni kuona watoto wengi wa kike wanamaliza shule, wanafaulu na kujiamini kuendeleza maisha yao.

Chanzo - Mwananchi

Post a Comment

0 Comments