Katika mechi ya leo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Mbeya City, Mbeya City wameibuka na ushindi kwa kuichapa Ruvu bao moja kwa bila.
BAO la Baraka Mwalubunju dakika ya 67 limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 35 na kupanda nafasi ya saba, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 28 nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi 28 sasa.

0 Comments