YANGA WAMTAKA CHAMA KWA NGUVU,SIMBA WAGOMA...MVUTANO WAIBUKA...


YANGA kupitia kwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mbata imethibitisha kuwasiliana na Berkane ya Morocco kuangalia uwezekano wa kumsainisha Clatous Chama.

Lakini akaenda mbali zaidi kwa kusisitiza kwamba si Chama tu hata staa yoyote wakimtaka kwenye dirisha dogo wanampata na mkwanja wanao wa kutosha Jangwani.

Staa huyo wa Zambia aliuzwa na Simba kwa Berkane hivikaribuni, huku ikielezwa kuwa kwenye mkataba wake wa miaka mitatu kuna kipengele kinachoibeba Simba. Inaelezwa kuwa Berkane wakitaka kumuuza lazima wawasiliane na Simba kwanza kama wanamtaka au hawamtaki kabla ya kumuuza pengine.

Kwa mujibu wa rekodi za soka, mkataba kama huo wa Chama wa vipengele vya mauziano(Buy Back Clause) uliwahi kuwahusu Memphis Depay alipouzwa na Man United kwenda Lyon na Alvaro Morata alipouzwa na Real Madrid kwenda Juventus ya Italia.

Lakini Senzo alidai kuwa wanajua ubora wa Chama lakini kwasasa wanaiheshimu klabu yake ya RS Berkane na kwamba tayari Yanga imeulizia uwezekano wa kumpata na hawajapata jibu rasmi huku dirisha dogo la usajili likifunguliwa Desemba 15.

“Chama ni mchezaji bora hakuna klabu ambayo itakataa kuwa naye na kwasasa tunaiheshimu Berkane kwa kuwa bado wanamkataba naye lakini nikweli tumeulizia uwezekano wa kumpata na kama kutakuwa na uwezekano wa kumleta hapa tutamleta,”alisema Senzo ambaye alifanya kazi na Chama wakiwa Simba.

Senzo alisema hata hivyo Yanga yao ya sasa haiko katika unyonge wa kumkosa staa yoyote ambaye wanamtaka hasa akipendekezwa na benchi lao la ufundi au kamati ya usajili.

Alisema jeuri yao hiyo inatokana na uimara wa uongozi wao lakini pia uwepo wa wafadhili na wadhamini wao GSM ambao haoni kama kuna timu kwasasa inaweza kuwapokonya mchezaji kama wakimtaka.

“Tulikua na maisha hayo huko nyuma lakini Yanga ya sasa sio rahisi ushindane nayo kutaka kumchukua mchezaji kisha ukafanikiwa kwuazidi tuna ushawishi mzuri na nguvu ya fedha.

“Unapokuwa na uongozi unaosimamia misingi mizuri ya soka na malengo kisha kubwa zaidi ukawa na watu kama GSM unakuwa na nguvu ya kutrosha kumchukua mchezaji yoyote ambaye unamtaka hapa ndani na hata nje.

“Ukifuatilia wako wachezaji wengi ambao walitakiwa na klabu zingine lakini baadae wakawakosa wakizidiwa na Yanga,hii ina maana kwamba GSM ambao ni wananchi sio rahisi kuwashinda linapokuja suala la Yanga inahitaji kitu.

“Tuna benchi la ufundi lakini pia tuna kamati ya ufundi hizi idara mbili zinazoshirikiana kwa karibu kufanya kazi hii ya kutengeneza timu na utakumbuka walitulia msimu huu na sasa tunafanikiwa wachezaji tuliowasajili walitokana na mapendekezo ya makocha na watu wa ufundi.

SIMBA WASHIKILIA MPINI
Mmoja wa viongozi wa Simba jana aliliambia Mwanaspoti kwamba Yanga wanajifurahisha kwani kwa mujibu wa makubaliano ya Mnyama na Berkane, Chama hawezi kuuzwa popote ndani ya miaka mitano ijayo bila Simba kuhusishwa.

Alidai kwamba kama wao watakuwa hawamhitaji Chama ndipo watawaruhusu Berkane kumuuza popote, lakini si ndani ya ardhi ya Tanzania. Lakini rekodi zinaonyesha ni ngumu watani hao wa jadi kuuziana staa kama huyo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.