MTOTO MCHANGA WA SIKU TANO AOKOLEWA NA PAKA MUMBAI

Mtoto wa kike wa siku tano, ambaye aliokolewa kutoka kwenye shimo la maji taka alimokuwa ametupwa jijini Mumbai, India anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya eneo hilo.

Madaktari katika hospitali ya Rajawadi wameambia BBC kuwa "anaendelea vyema" na kwamba afya yake inafuatiliwa kwa karibu.

Polisi wanasema wakaazi walimpata mtoto huyo baada ya kundi la paka waliokusanyika kando ya barabara na kuanza kuzua fujo - na kupiga kelele kwa sauti ya juu.

Maafisa wanachunguza jinsi alivyoishia kwenye bomba hilo.

Polisi hawajatoa tamko lolote kuhusiana na kile kilochochangia tukio hilo lakini matukio mengine kama hayo siku za nyuma yamehusishwa na suala la watoto wa kiume kupendelewa zaii kuliko wa kike nchini India.

Wanawake mara nyingi wanabaguliwa kijamii na wasichana wanaonekana kama mzigo wa kifedha, haswa miongoni mwa jamii masikini.

Uwiano wa kijinsia wa nchi ni mojawapo ya hali mbaya zaidi duniani. Na ingawa mimba zinazokadiriwa kuwa za watoto wa kike hutolewa kwa usaidizi wa kliniki haramu, visa vya watoto wa hao kuuawa au kuachwa baada ya kuzaliwa si jambo la kushangaza.

Katika tukio la hivi punde zaidi, mtoto huyo aliokolewa na timu ya polisi inayoongozwa na wanawake kutoka kitongoji cha Mumbai siku ya Jumapili.

Chanzo - BBC

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.