KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA...RUVU SHOOTING 'WAJICHUA' KWA MASAA MANNE JUANI..

SAA nne zimeitosha timu ya Ruvu Shooting kujifua na kujiandaa kwa mchezo wa keshokutwa dhidi ya Simba utakaopigwa saa 10 Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ruvu ambao ni wenyeji wa mchezo huo waliwasili uwanjani hapo saa 9:30 alasiri na kuanza mazoezi dakika 20 baadae na kumaliza saa 12:30 jioni.

Kocha Mkuu Boniphace Mkwasa alianza kwa kuwapa maelekezo vijana wake kile anachokitaka na wanachopasa kuzingatia.

Timu hiyo ilianza kwa mazoezi ya kukimbia kusaka pumzi wakitumia dakika 40, kupiga pasi, kumiliki mpira ambapo alihakikisha anasimamisha mazoezi na kutoa maelekezo upya pale mchezaji alipofanya makosa.

Mkwasa alifanya hivyo pale Pius Buswita alipokosea kutuliza mpira na kutoa pasi mkaa, ambapo kocha alisimamisha tizi na kumuita akimuuliza shida ni nini huku akisikika kutoa maelekezo akisema 'Keep the ball'.

Baada ya Ruvu kuhitimisha mazoezi yake Mratibu wa Simba, Abbas Ally na Katibu wa tawi la Simba mkoa wa Mwanza Filbert Kabago wakiongozana na Meneja wa Uwanja huo waliingia katikati ya uwanja wakiukagua huku Meneja huyo akiwaonesha maeneo mbalimbali ya eneo la kuchezea lilivyo tayari kwa mechi.

Abbas amesema msafara wa Simba ungewasili jijini Mwanza saa 3 usiku wa jana na leo asubuhi timu itafanya mazoezi uwanjani hapo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.