KAZE AUMIA SANA KUHUSU YANGA, AWAFUNGUKIA WACHEZAJI MAMBO MAZITO
Kocha Msaidizi wa Young Africans Cedric Kaze amesema endapo wanahitaji kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu huu 2021/22, kikosi chao kinapaswa kupambana katika viwanja vizuri na vibovu.
Kaze ametoa rai hiyo kwa wachezaji wa Young Africans, baada ya kuambulia alama moja dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa mzunguuko wa sita wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumamosi (Novemba 21), Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.
Kaze ambaye alikua Mkuu wa Benchi la Ufundi klabuni hapo kabla ya kutimuliwa mwishoni mwa mwaka 2020 na kisha kurejea kama Msaidizi wa Kocha Nabi amesema: “Kama tunahitaji ubingwa inabidi wachezaji wetu waweze kucheza kwenye viwanja vya aina zote, vizuri na vibovu, hivyo inabidi sasa tujielekeze kuwafundisha jinsi ya kucheza kwenye aina mbalimbali za viwanja, lakini pamoja na hayo tunashukuru kwa kupata pointi moja, tunakwenda kujipanga.”
Sare ya 1-1 dhidi ya Namungo FC imeifanya Young Africans kufikisha alama 16 zinazoendelea kuwaweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, huku Simba SC ikifuatia kwa kuwa na alama 14.
Young Africans itarudi tena Uwanjani juma lijalo (Novemba 30), kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza FC itakayokua nyumbani Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, huku Simba SC ikitarajia kucheza dhidi ya Geita Gold FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: