Breaking News: MAAMUZI KESI YA MORRISON DHIDI YA YANGA YATOLEWA, MAAMUZI YAKO HIVI...

MCHEZAJI wa Simba, Bernard Morrison ameshinda kesi ilipelekwa na klabu ya Yanga katika mahakama ya usuluhishi wa Michezo (CAS).

Yanga walipeleka kesi hiyo CAS baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya kamati ya haki na maadili na hadhi ya Wachezaji ambayo ilitoa hukumu kuwa mkataba wa Yanga na Morrison ulikuwa na mapungufu hivyo ikaruhusu usajili kwenda Simba.

Kwa upande wao Yanga wamekuwa wakisisitiza kuwa Morrison ni mchezaji wao halali. Morrison alisajiliwa Yanga katika dirisha dogo 2019/2020, ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa kabla ya kutimkia Simba.



Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.