BAADA YA SIMBA KUFANYA YAKE, YANGA WAKAA KIKAO KIZITO.... WAJADILI JAMBO HILI
Viongozi wa Yanga wakiongozwa na mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM, injinia Hersi Said jana walifanya na wachezaji kwa dakika 15 baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi.
Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Ilulu kuanzia Saa 10:20 jioni na kumalizika, Saa 12:00, baada ya mazoezi hayo Hersi na baadhi ya viongozi waliwataka wachezaji wote kubakia ndani ya Uwanja.
Wachezaji na viongozi hao walizunguka duara huku Hersi akionekana pekee akiongea kama anawasisitiza jambo fulani, kikao kilichochukua muda wa dakika 15.
Baada ya kumalizika kikao hicho wachezaji na benchi la ufundi walionekana kufurahi na wengine wakionekana kuangua kicheko kisha kutoka ndani ya Uwanja kuelekea kwenye gari.
Wakati wakitoka ndani ya Uwanja, mashabiki waliokuwa wameruhusiwa kuingia ndani baada ya mazoezi waliwashangilia huku mchezaji aliyewateka zaidi akiwa ni Feisal Salum' Fei Toto' na Fiston Mayele ambao walishangiliwa sana na wengine kuwaomba kupiga nao picha.
Hersi hakutaka kuweka wazi alichowaambia wachezaji katika kikao hicho lakini akawataka mashabiki kufika kwa wingi kesho kuishangilia timu yao kwani anaamini watapata ushindi.ADVERTISEMENT
"Mechi ya Namungo itakuwa ngumu kwani wamefanya usajili mzuri na pia wana uongozi mzuri lakini hata sisi tumejipanga kwani tuna kikosi bora na tunataka tuendeleza ushindi ili tuzidi kukaa kileleni kwenye msimamo wa Ligi" amesema Hersi ambaye ameingia hofu na hali ya Uwanja kuwa hauna ubora.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: