KUELEKEA MECHI DHIDI YA AZAM JAMBO JIPYA LAIBUKA YANGA
MMOJA wa viungo waliotamba na Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000, Tito Andrew amesema mastaa wa kikosi hicho, washindwe wenyewe kunyakua taji la Ligi Kuu Bara msimu huu, kutokana na kikosi bora walichonacho.
Andrew alisema mastaa wa Yanga, wana morali ya kazi inayotokana na kujiamini na ni mtaji mkubwa wa kuwasaidia kukaa mstari wa ubingwa 2021/22 kwani akiangalia timu zingine anaona zina mapungufu.
Staa huyo wa zamani wa Taifa Stars na Moro United, alisema “Yanga ilianza kufunga bao moja moja, kisha mabao 2-0 dhidi ya KMC, inaonyesha ni namna gani kocha Nabi anavyotengeneza kikosi chake kuwa tishio, jambo la msingi wawe na muendelezo.”
“Morali ya wachezaji wa Yanga ipo juu, wachezaji wanaoonyesha kuna kitu wanakihitaji kwa msimu huu, huwezi kuwafananisha na Simba ambao kikosi chao hakijakaa sawa baada ya kuondoka Luis Miquissone na Clatous Chama,” aliongeza. Alisema anaitazama Yanga kiufundi zaidi na hashangazwi wanapokuwa wa moto kipindi cha kwanza, ambacho ndicho walichofunga mabao yao.
“Nabi kiufundi timu yake kupata matokeo kipindi cha kwanza yupo sawa, ingawa akishinda cha pili siyo dhambi, ligi bado ni ndefu anapopata pointi tatu anawapumzisha wachezaji wasitumie nguvu kubwa itakayowagharimu kushindwa kufanya vibaya mechi inayofuata,” alisema Andrew na kuongeza; “Mfano Simba wangetumia mfumo huo wa Nabi, wasingetolewa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani baada ya kupata bao kipindi cha kwanza wangelilinda, unaweza ukaelewa ninaposema huwezo kufananisha morali ya Yanga na Simba,”alisema.
Kauli yake iliungwa mkono na beki wa zamani wa timu hiyo, Oscar Joshua aliyesisitiza “Ukiangali viungo wakabaji kuna Mukoko, Mauya na Aucho wote ni wachezaji wenye uwezo wa juu, jambo ambalo Simba kwa sasa halipo, ndio maana nasema ni wakati wa Yanga kuchukua mataji hayo,” alisema.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: