WAZIRI WA MAMBO YA NJE AJIUZULU BAADA YA SERIKALI KUSHINDWA KUPAMBANA NA RUSHWA
Waziri wa Mambo ya Nje, Harry Kalaba, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, kwa kile alichodai kushindwa kwa Rais wa Zambia Edgar Lungu, kupambana na rushwa.
Kalaba amesema uamuzi wake umetokana na kiwango cha juu cha rushwa ambayo inafanywa na watu ambao wanatarajiwa kuwa suluhisho katika taifa hilo.
Amesema tayari amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Lungu na kwamba amechukua uamuzi huo kwa moyo mzito, hata hivyo Msemaji wa Rais, Amos Chanda, amesema Ikulu bado haijapokea barua ya kujiuzulu kwa Kalaba.
Kalaba anakuwa Waziri wa tatu kuondoka ndani ya serikali ya Rais Lungu baada ya kutimuliwa kwa Mawaziri wawili akiwemo Waziri wa Mipango na Waziri wa Habari na Utangazaji.
Kalaba, ambaye ni Mbunge wa chama tawala cha Patriotic Front (PF), anatajwa kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka 2021 ikiwa Lungu atajiweka pembeni.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: