YANGA NAO WAAMUA KUIIGA SIMBA JUU YA UENDESHAJI

Klabu ya Yanga iko mbioni kufanya mabadiliko ya uendeshaji ikiwa ni siku moja baada ya klabu ya Simba kuandika historia ya kubadili mfumo wake wa uendeshaji.

Akihojiwa na moja ya redio maarufu nchini, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema tayari kikao cha Kamati ya Utendaji kimeitishwa kuandaa maandalizi ya mchakato huo.

"Sisi kama Yanga tumeitisha kikao cha kamati ya utendaji, Katiba yetu inatoa mwanya kuanzisha kampuni itakayomilikiwa na klabu, ambapo kampuni itamiliki asilimia 49 ya hisa, huku 51 zikimilikiwa na wanachama," amesema Sanga.

Hii si mara ya kwanza kwa Yanga kuanzisha mchakato wa kufanya maadiliko.

Mwenyekiti wa zamani wa Yanga ambaye alijiuzulu, Yusuf Manji mwaka jana alitangaza azma yake ya kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10 wakati akifanya mkutano mkuu wa dharula na wanachama wa klabu uliofanyika Agosti 6 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee eneo la Upanga jijini Dar es Salaam.

“Nitaikodisha kwa asilimia 75 na 25 inabaki kwa wanachama. Nataka kuikodisha timu na nembo, majengo ya klabu yanabaki kuwa mali ya wanachama.

“Katika miaka 10, ikipatikana faida 25 inakwenda kwa wanachama na klabu na 75 kwangu. Kama itakuwa ni hasara basi inakuwa hasara yangu, hakuna hasara upande wa wanachama au klabu,” alisema.

“Tayari nimewasilisha ombi hilo Bodi ya Wadhamini ambao wao watazungumza na nyinyi wanachama na kama kutakuwa na makubaliano basi tutaingia mkataba,” alisema Manji.

Pia Manji alisema masuala ya timu kuhusu usajili, mishahara, uendeshaji kama safari na gharama nyingine zitakuwa chini yake.

Pia asilimia 25 ambayo itakuwa ni ya klabu, ndiyo itatumika kuujenga Uwanja wa Kaunda na Yanga itakuwa na uwanja wa kufanyia mazoezi na ikiwezekana hata kuchezea mechi.

Hata hivyo mpango huo ulikwama baada ya baadhi ya wanachama wakiongozwa na Mzee Akilimali kuupinga vikali.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.