STAND UNITED YAMSAJILI NDEKUMANA, YAWAPIGA CHINI WA VIJIJINI


KLABU ya Stand United maarufu kama 'Chama la Wana' limesajili kwa mpigo wachezaji watatu na wawili kati yao ni Warundi na wameachana na wale 'wakulima' waliosajiliwa kutoka vijijini, eti kazi yao ilikuwa ni kushangaa magorofa tu.

Stand imewasajili Warundi Ndekumana Seleman ambaye ni mshambuliaji anatoka Vital'O ya Burundi kwa mkataba wa miezi sita na Bilimana Bleys ambaye alikuwa anacheza Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na mzawa Abdallah Juma aliyekuwa anaichezea Mbeya City.

Katibu wa timu hiyo, Kenny Nyangi alisema: "Lengo la kufanya usajili huo ni kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zilizobaki."

"Tumemsajili, Abdallah Juma alikuwa majeruhi lakini sasa amepona, tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwetu, lakini pia kocha amesema hawezi kuendelea kuwatumia wachezaji ambao tuliwasajili kutoka vijijini, ametaka wapelekwe timu za madaraja ya chini,"alisema Nyangi.

Wachezaji waliosajiliwa chini ya kocha, Athuman Bilali 'Bilo' ni Amblosi Jamse Mganda, Mageta Paul, Kisatya Gillevan, Songa Beteli, Salva Mkulila, Said Mbati, David Mwita, Martius Mahalu na Wille Charles.

"Tumeona tuwapunguze kabla hatujafika jijini Dar es Salaam kucheza na Simba, Yanga na Azam, maana kama wanashangaa mikoa midogo itakuaje huko mjini, kocha alisema amechoka kufanya nao kazi,"alisema.

"Ndio maana tumewasajili wachezaji wazoefu ambao watakuwa msaada kwa timu na siyo kama tulivyoanza, leo wanacheza vizuri, mechi inayofuata tia tia maji, hii ni hatari."

CREDIT-MWANASPOTI

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.