SIRI YA DK. CHAELES KIMEI KUNG'OKA CRDB HII HAPA
Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi Wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kuanza kwa mchakato wa kumtafuta mkurugenzi mpya wa benki hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Tully Mwambapa. Picha na Loveness Bernard***************
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, ametangaza kustaafu nafasi yake ndani ya benki hiyo.
Dk. Kimei anakuwa kiongozi wa pili kutangaza uamuzi huo mgumu baada ya Mei 20, mwaka huu Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, kutangaza kujiuzulu ujumbe wa bodi wa benki hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk. Kimei alisema kuwa ameamua kulieleza hilo mapema na ifikapo Mei 31, 2019 atang’atuka rasmi na kumwachia kijiti mtu mwingine. Atakuwa ameiongoza benki hiyo kwa miaka 21.
Dk. Kimei ambaye amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo tangu mwaka 1998, alisema amechukua uamuzi wa kutoongeza mkataba mwingine kwa hiyari yake na anaamini kuondoka kwake, benki itaendelea kuwa imara huku yeye akibaki kuwa mteja na mwanahisa.
“Kunaweza kuwa na hisia mbalimbali, lakini mimi mwenyewe nimeamua kutoongeza muda wa mkataba. Hadi nitakapoondoka nitakuwa nimekaa miaka 21 na ninamshukuru Mungu sana kwa sababu miaka hii ni mingi, na huwezi kukaa miaka yote hiyo bila kukabiliana na changamoto mbalimbali.
“Ni vizuri kuwaachia wengine ili waweze kuendeleza… nitabaki kuwa mwanahisa na mteja wa benki,” alisema Dk. Kimei.
MTANZANIA
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: