SIMBA YAPATA MSHAMBULIAJI KUTOKA MWADUI FC
HARAKATI za usajili wa wachezaji katika vilabu vya soka la Tanzania, zinaendelea kwa nguvu huku Klabu ya Simba ikikaribia kumsajili shambuliaji wa Mwadui FC, Hassani Kabunda katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, hiyo inafuatia mazungumzo baina ya timu hizo mbili kwenda vizuri.
Kabunda amezungumza na chombo kimoja cha habari na kusema kwa namna Simba, walivyo kamia muda wowote anaweza kumalizana na viongozi wa timu hiyo na yeye kuwa mali ya Simba
“Nafurahi kuona timu kubwa kama Simba, inataka kunisajili mimi hiyo ni habari njema kwangu kwa sababu Simba ni timu kubwa hivi kujiunga nao naamini kutaongeza maslahi lakini pia kutoa mchango wangu kwa timu ambayo naichezea kwa upendo,” alisema mchezaji huyo.
Kabunda aliongeza kuwa ili awe na amani Simba anataka kucheza kwa malengo na kuwa tegemeo kikosi cha kwanza lakini ameitaka Simba imboreshee maslahi, yawe mazuri zaidi ya anayoyapata Mwadui FC.
Amesema kwa sasa mpira ni kazi, kwa hiyo hata dau kubwa ni sehemu ya ushawishi kwa mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine lakini kwake muhimu zaidi ni uhakika wa kucheza.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: