SAID KUBENEA AFUNGUKA JUU YA TAARIFA ZA KUHAMA CHADEMA
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema hana sababu za msingi zinazomfanya kujiuzulu nafasi hiyo.
Pia, amewaonya wanaoeneza uzushi huo akitaka waache tabia hiyo.
Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani amesema leo Jumatano Desemba 6,2017 saa saba mchana katika ofisi za kanda hiyo Magomeni Dar es Salaam, atakuwa na mkutano na waandishi wa habari.
Ametoa kauli hiyo baada ya taarifa kuenea kuwa ni miongoni mwa wabunge wa upinzani watakaohama vyama vyao katika dhana ya kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.
Akizungumza na MCL Digital, Kubenea amesema hajawahi kumweleza yeyote kwamba ana mpango wa kuhama na hafikirii kufanya hivyo.
Mwananchi
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: