HIZI HAPA PICHA ZA MAKAZI MAPYA YA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU MJINI DODOMA

Makamu wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amehamia rasmi mjini Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli, la kuhamishia serikali katika Mji Mkuu wa Dodoma.

Mama Samia Suluhu akiongea wakati wa hafla fupi ya kukaribishwa Dodoma iliyofanyika katika makazi yake, amewashukuru wananchi wa Dodoma kwa kumpokea na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya nchi.

Makamu wa Rais ameeleza kuwa ili kuhakikisha kuwa wanadumisha mazingira na kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani siku ya Alhamisi, Disemba 21, mwaka huu itakuwa ni siku ya kushiriki upandaji wa miti na yeye atapanda mti wa mjini hapo.



    

  
SWAHILI TIMES

Post a Comment

0 Comments