HATIMA YA DHAMANA YA WABUNGE WAWILI WA CHADEMA KUJULIKANA LEO... NI BAADA YA JANA KURUDISHWA RUMANDE

Wabunge Susan Kiwanga na Peter Lijualikali waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro pamoja na washtakiwa wengine 36 walirejeshwa rumande.

Mahakama iliyokuwa itoe uamuzi wa dhamana jana Jumanne Desemba 5,2017 ilikwama kufanya hivyo kutokana na kuibuka hoja za kisheria.

Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unavutana kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo.

Kutokana na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack aliahirisha kesi hiyo hadi leo Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili kujibu hoja kuhusu hati hiyo.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.

Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.

Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Frederick Sumaye walihudhuria mahakamani.

Wengine waliofika mahakamani ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wa Viti Maalumu, Devota Minja.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.