HABARI MPYA ZILIZOTUFIKIA JIONI HII 1/12/2017 KUTOKA YANGA
IKIFIKA Jumatatu ya Desemba 4, Yanga itakuwa na mastraika wapya watatu ambao kazi za miguu yao zitatoa jibu la kwamba wakatwe wa kigeni wawili au mmoja.
Mshambuliaji wa kwanza ambaye Mwanaspoti lilikutajia ni yule Bensua Da Silva ambaye ni raia wa Guinea Bisau mwenye asili ya Ivory Coast wikiendi hii atatua nchini tayari kwa majaribio hayo chini ya kocha George Lwandamina ambaye aliwapa bata la siku saba wachezaji wake.
Mshambuliaji wa pili ni yule tuliyekwambia katika toleo letu la jana Badara Kella raia wa Sierra Leone akiwa ni mchezaji pekee wa anayecheza ligi ya ndani mwenye uhakika katika kikosi cha kwanza cha taifa lake.
Mbali na hao kifaa cha tatu ni Mghana, Adam Zikiru ambaye naye anakuja kwa mualiko kwa benchi la ufundi akitokea Ligi Kuu ya Zambia na wikiendi hii inatia mguu Bongo.
Kilichowavutia Yanga kwa Zikiru ni rekodi yake nzuri ambapo katika mkataba wa miezi sita katika klabu ya Nchanga Rangers amefunga mabao 11 katika mechi 12 ambapo Yanga inataka kuwazidi kete Wazambia hao ambao wanajipanga kumpa mkataba mrefu.Mchujo wa washambuliaji hao utafanyika ndani ya wiki moja pekee ambapo Yanga italazimika kufanya mambo yake kwa haraka kabla ya dirisha dogo kufungwa Desemba 15.
Anakatwa nani?
Upepo hauko vizuri kwa Donald Ngoma ambaye amesharejea nchini na jana Alhamisi alionekana akifanya matanuzi mida ya mchana kwenye kiwanja kimoja ndani ya Mlimani City.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: