BAADA YA KURUDI CCM WEMA SEPETU ADAI KUKATISHWA TAMAA

Baada ya msanii wa filamu, Bongo Wema Sepetu kurudi CCM kutokea Chadema, hatimaye amevunja ukimya na kufunguka ya moyoni.

Wema amesema hawezi sana kulizungumzia hilo kwa sababu maamuzi yalishafikiwa lakini anajihisi kukatishwa tamaa.

“Yaani it so complicated najikuta sipo kwenye position ya kuielezea in simple English or Swahili, siwezi lakini tubaki tu tunaomba Mwenyenzi Mungu kwamba everything it will be ok one day inshallah” Wema ameiambia K Fm, Rwanda.

“I am strong, nisingekuwa strong nisingekuwa hapa sasa hivi najaribu kusali kwa hii hali, muda mwingine kama bidamu inakuwa inanivunja moyo najihisi nimekatishwa tamaa, yaani ok! acha nimuachie Mungu” ameongeza.

February 24 mwaka huu Wema alijiunga na Chadema akitokea CCM na December Mosi alitangaza kurudi CCM.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.