ASKOFU EMMANUEL MAKALA AZINDUA MNARA WA MAADHIMISHO YA MIAKA 500 YA MATENGENEZO YA KANISA KKKT SHINYANGA

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini mashariki ya Ziwa Victoria, Dk. Emmanuel Joseph Makala, leo Jumapili ya tarehe 10/12/2017 amezindua mnara alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo KKKT duniani katika Usharika wa Ebeneezer Kanisa Kuu Shinyanga.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Askofu Makala amesema mnara huo ni alama iliyobeba ujumbe wa matengenezo ya kanisa ikiwa na maana wokovu wa mwanadamu unapatikana kwa NEEMA TU, NENO TU na KRISTO TU yaliyoletwa na Martine Luther katika mapinduzi ya kanisa yaliyofanyika mwaka 1517 na Martine Luther huko Ujerumani alipotundika hoja 95

Maadhimisho hayo yaliambatana na ibada ya ubarikio wa kipaimara wa watoto 107 wa Usharika huo ambapo Askofu Makala amewaasa na kuwataka watoto hao kumtumikia Mungu katika roho na kweli kwani huu ndio wakati wao wa kuanza kumtumikia Mungu.

Akizungumzia msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa wafungwa 1828 akiwemo Babu Sega na mwanae Papii Kocha, Askofu Makala amesema jambo hilo ndio maadhimisho halisi ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa kwani kilichotolewa na mheshimiwa Rais ni NEEMA TU.

Maadhimisho haya kikanisa (kitaifa) yalifanyika tarehe Oktoba 1-8 2017 jijini Arusha
Mnara wa alama ya matengenezo ya Kanisa ukiwa bado haujazinduliwa
Akofu Dk. Emmanuel Makala akizungumza machache na washarika juu ya mnara huo kabla ya kuuzindua rasmi
Askofu Dk. Emmanuel Makala akiendelea kutoa ufafanuzi zaidi kwa washarika juu ya maadhisho ya miaka 500 ya matengenezo ya Kanisa
Msaidizi wa Askofu Trafaina Nkya (wapili kutoka kulia), Wachungaji na mashemasi wakimsikiliza askofu Makala akielezea juu ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa wakati wa uzinduzi wa mnara wa alama ya madhimisho hayo
Askofu Makala akiendelea na uzinduzi wa mnara wa alama ya maadhimisho ya matengenezo ya kanisa
Askofu Makala akiendelea na uzinduzi wa mnara wa alama ya maadhimisho ya matengenezo ya kanisa
Askofu Dk Emmanuel Makala akikata utepe ikiwa ni alama ya uzinduzi wa mnara wa maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa
Askofu Dk. Emmanuel Makala akielezea machache mara baada ya kuzindua mnara wa alama ya matengenezo ya kanisa ya miaka 500
Mwoneekano wa mbele wa mnara wa alama ya maadhimisho ya matengenezo ya kanisa ya miaka 500
NEEMA TU (Ujumbe mojawapo wa mnara wa alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa)
IMANI TU (Ujumbe mojawapo wa mnara wa alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa)NENO TU (Ujumbe mojawapo wa mnara wa alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa)

Isaac Luhende - MASENGWA BLOG

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.