Breaking News : DAVID KAFULILA AJIONDOA CHADEMA



Mwanasiasa maarufu wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini David Kafulila leo Jumatano Novemba 22,2017 ametangaza kujivua uwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa kile alichosema hana imani na vyama vya upinzani kama jukwaa salama la kupambana na ufisadi nchini Tanzania. 


Kafulila amejiondoa CHADEMA na baada ya maamuzi hayo ameeleza sababu kwamba kwa sasa vyama vya upinzani vinaonekana kupigwa ganzi na kupooza katika juhudi zake za kupambana na ufisadi na ghafla ufisadi siyo agenda kuu tena ya vyama vya upinzani tena. 


“Kwa kuwa sina imani tena na upinzani kama jukwaa salama la kupambana na ufisadi, nimeamua kwa hiari na utashi wangu kujivua uanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe ya taarifa hii, nitatangaza kwa siku za hivi karibuni jukwaa jipya la harakati zangu dhidi ya ufisadi”- Kafulila

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.