LULU MICHAELE AIELEZA MAHAKAMA JINSI ALIVYOGOMBANA NA KANUMBA NA JINSI ALIVYOFARIKI
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael (Lulu), imeendelea leo ambapo upande wa mshtakiwa umeanza kutoa utetezi wake.
Akisimulia jinsi ilivyokuwa siku ya tukio, Lulu amesema marehemu alikuwa akimpiga na panga baada ya kutokea ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi, alipomuona akiongea na simu.
"Nilikuwa nataka kutoka ila marehemu 'Kanumba' alinikataza, alikuwa hataki nitoke, nilipomwambia natoka na marafiki zangu alinikimbiza na taulo na mimi nilikuwa naogopa kupigwa, mara nyingi alikuwa ananipiga kila akilewa na sio kwa akili zake, alipoona simu yangu inaita akahisi ni simu ya mwanaume akasema kwanini naongea na simu ya mwanaume mbele yake? Marehemu akaingia uvunguni akatoa panga akasema leo nakuua huku akinipiga na panga kwenye mapaja", ameelezea Lulu.
Lulu ameendelea kusimulia...."Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa, nilimwambia Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka akasema anaenda kumuita daktari, alivyosema anaenda kumuita daktari na mimi nikaondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga, niliondoka nikawasha gari kuelekea Coco Beach kutuliza akili".
Muigizaji huyo ameendelea kusimulia kwamba ..."Nilivyofika Coco beach meseji zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki, nikampigia 'Kidume' ambaye ni rafiki yake Kanumba kumuuliza Kanumba yupo hospitali gani niende kumuona, akaniambia wewe usije hospitali, niambie uko wapi, tukakubaliana tuonane Bamaga, tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata".
Pamoja na hayo muigizaji huyo ameithibitishia mahakama kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu (Steven Kanumba) kwa muda wa miezi minne kabla ya kukutwa na mauti.
Mahakama Kuu imeghailisha kesi hiyo mpaka siku ya kesho Oktoba 24, ambapo itasikilizwa tena

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi