EMMANUEL OKWI ALIA NAMWAMUZI,AWAPA NENO ZITO YANGA

Mshambuliaji kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi, amemlaumu mwamizi Elii Sasii, kwa kushindwa kumlinda kutokana na rafu alizokuwa akichezewa na mabeki wa timu ya Yanga.

Okwi amesema mabeki wa Yanga, Kelvin Yondani na Endrew Vicent ‘Dante’, walistaili kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na rafu za mara kwa mara walizokuwa wakimchezea kwenye mchezo huo.
“Nilimlalamikia mwamuzi mara kwa mara kumtaka awe makini na wachezaji wale lakini chakushangaza mwamuzi aliendelea kuwaangalia na kushindwa kutoa hata kadi ya njano kwa mmoja wao jambo ambalo liliwapa uhuru wa kuendelea kucheza ndivyo sivyo,”amesema Okwi.
Mshambuliaji huyo mwenye mabao nane hadi sasa amesema kwa kiwango alichokuwa nacho hadhani kama Yanga wanauwezo wa kuizuia Simba pindi wanapotaka jambo lao na sare ya juzi ilitokana na msaada kutoka kwa mwamuzi huyo.
Amesema alikuwa na hamu ya kuifunga Yanga, juzi lakini baada ya kushindikana anaiweka hamu yake na kusubiri mchezo wa marudiano ambao utachezwa mwakani na kutamba kuwa atahakikisha anawafunga.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.