HABARI MPYA NA YA KUSISIMUA KUTOKA KLABU YA SIMBA
Klabu ya Simba, kesho siku ya Jumanne tarehe 31/10/2017 tunataraji kuwa na mkutano na vyombo vya habari.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano ulipo makao makuu ya klabu, kuanzia majira ya saa 6 mchana.
Katika mkutano huo,mambo mengi ya msingi yatazungumziwa na kutolewa ufafanuzi na Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Haji S. Manara.
Hivyo tunawaomba waandishi wote wa habari za michezo kufika bila kukosa kwa kuzingatia muda tajwa hapo juu.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba Sports Club.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi