MFUNGAJI WA YANGA DHIDI YA SIMBA MECHI YA JUMAMOSI OBREY CHIRWA AFUNGUKA MAZITO

Mshambuliaji nyota wa klabu ya Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa amefunguka na kueleza furaha yake baada ya kufunga kwa mara ya kwanza katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba tangu atue klabuni hapo akitokea FC Platinum ya Zimbabwe.

Chirwa ambaye amepitia Changamoto mbalimbali kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga ikiwemo kubezwa kuwa kiwango chake hakiendani na thamani yake ambayo ilitajwa kuwa ni shilingi milioni 200 amedai bao hilo dhidi ya Simba limemwongezea morali ya kufanya vizuri zaidi.

“Nina furaha kubwa kuweza kufunga goli katika mechi kubwa dhidi ya Simba, ni bao muhimu sana kwangu, goli hili linanifanya niongeze morali ya kutaka kufunga magoli zaidi”, amesema Chirwa.

Aidha Chirwa ameongeza kuwa katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi dhidi ya Simba alijitahidi kadri ya uwezo wake ili afunge goli lakini mlinda mlango wa Simba alikuwa imara kuokoa mipira yake hadi pale alipofanikiwa kufunga dakika ya 60.

Chirwa amefikisha magoli 3 na kutengeneza mengine 2 kwa Ibrahim Ajibu na kumfanya awe mchezaji muhimu sana msimu huu ndani ya kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa ligi kuu. Msimu uliopita Chirwa alifunga magoli 12.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.