Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Taarifa hii imekuja baada ya jana Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe kupitia mtandao wa Twitter kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwamba nini kimetokea mpaka ndege nyingine aina ya Bombardier iliyotakiwa kuwasili nchini mwezi Julai kutowasili nchini mpaka sasa.
Profesa Mbarawa alimjibu kwamba kuna taratibu za mwisho zinafanywa kabla ya ndege hiyo kuwasili nchini, lakini itawasili





