TUNDU LISSU APANDISHWA MAHAKAMANI MAWAKILI 21 WAJITOKEZA



Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (KATIKATI), alivyofikishwa mahakamani.
Baada ya kuwekwa mahabusu kwa siku nne, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alifikishwa Mahakama ya Kisutu kusomewa mashtaka yanayomkabili.

UPDATES: Lissu alisomewa shitaka moja la kutumia maneno ya uchochezi wakati akihutubia kwenye mkutano Julai 17 mwaka huu jijini Dar.

Lissu anawakilishwa na mawakili 21 wakati serikali inawakilishwa mawakili 5. Aidha mawakili wa serikali wameomba Lissu anyimwe dhamana kwa kuwa ana mashauri matano mahakamani hapo yenye kesi za uchochezi, hivyo wamesema akiachiwa huru anaweza kudhuriwa.
Mawakili wa Lissu walipangua hoja hizo.