Makubwa Haya: MUME ALIYEHONGWA PESA AUA MKE WAKE AKIDAIWA KUHONGA MWINGINE
WATU wawili wamekufa katika matukio tofauti katika mkoa wa Rukwa, akiwemo mkazi wa Kijiji cha Mafulala Manispaa ya Sumbawanga, Anna Kashamsakula (35) aliyeuawa kikatili baada ya kuchinjwa na mumewe, baada ya kumtuhumu kumhonga mwanamke mwingine Sh 30,000.
Mshtakiwa alipewa fedha hizo na mkewe ili akalipe kodi ya jengo, waliyokuwa wakidaiwa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Rukwa.
Akithibitisha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema kuwa mauaji hayo yalitokea Julai 27, mwaka huu saa sita usiku katika kijiji chaMafulala.
Akifafanua, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi, ambapo marehemu alimpatia mumewe Sh 30,000 ili akalipie kodi ya jengo, ambapo hakulipa bali alienda kutumia na mwanamke mwingine.
Inadaiwa kuwa mume huyo alipewa kiasi hicho cha fedha na mkewe Julai 25, mwaka huu, lakini hakurudi hadi siku iliyofuata, ambapo ugomvi wa maneno uliibuka miongoni mwao hadi Julai 27, mwaka huu mume huyo alipoamua kumuua mkewe na kutokomea kusikojulikana.
IMEANDIKWA NA PETY SIYAME, SUMBAWANGA
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi