Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia viongozi 6 wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma kupitia chama hicho Mhe Zubeda Sakuro kwa tuhuma za kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa na kuzua vurugu wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema Dr. Mashinji amekamatwa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema“Tumepata taarifa kuwa katibu Mkuu amekamatwa dakika kama tano zilizopita tumepata taarifa kuwa katibu Mkuu amekatwa na kawekwa ndani kwa masaa 48”
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
