BAADA YA LIPUMBA KUMALIZANA NA WABUNGE WA VITI MAALUM, RUNGU KUHAMIA KWA WABUNGE WA MAJIMBO

Prof. Lipumba amesema, Kamati ya Maadili na Nidhamu ya chama hicho imeanza na wabunge nane wa viti maalamu na madiwani wawili, hivyo awamu ya pili, watahojiwa wabunge wa majimbo pamoja na Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho pamoja na wanachama wengine.

Wabunge 8 wa CUF waliovuliwa ubunge ni wabunge wa viti maalum wa chama hicho, na tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF), baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuiarifu tume kuwepo kwa nafasi hizo, kufuatiwa kutenguliwa kwa ubunge wa wabunge waliokuwa wanashikilia nafasi hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Ramadhan Kailima, imewataja wabunge hao kuwa ni, Rukia Ahmed Kassim, Shamsia Aziz Ntamba, Kizza Hussein Mayeye, Zainabu Mndolwa Amir, Hindu Hamis Mwenda, Sonia Juma Magogo, Afredina Apolinary Kahigi, na Nuru Awadhi Bafadhil.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.