BINTI ADAIWA KUNYONGA KITOTO KICHANGA CHA SIKU TATU KISHA KUKIZIKA

KAGERA: Katika hali isiyokuwa ya kawaida Binti mmoja anayeishi mtaa wa Ntungamo Kata ya Buhembe, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, Latifa Vedasto anadaiwa kumnyonga mtoto wake aliyejifungua siku tatu zilizopita na kisha kumzika 
Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi linamshikilia binti huyo mwenye umri wa miaka kumi na minane kwa uchunguzi zaidi baada ya kufukua shimo alilokuwa amezikwa kichanga huyo. 

Chanzo: TBC 1