USALAMA WANGU UMEKUWA MDOGO " ASEMA NAY

Msanii wa muziki wa hip hop ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Wapo’ Nay wa Mitego amedai kuna watu wanataka kumpoteza. 
Wiki moja iliyopita rapper huyo alikamatwa na jeshi la polisi kutokana na wimbo wake mpya ‘Wapo’. 

Hata hivyo Rais Magufuli alitoa tamko la kuachiwa kwa msanii huyo na kusema wimbo huo hauna matatizo. 

Rapper huyo Jumatatu hii amefunguka kwa kudai kuwa kuna watu wanamfuatilia kutaka kumpoteza. 

“Usalama wa maisha yangu umekua mdogo kwasasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii dunia.,” aliandika Nay wa Mitego Istagram. 

Aliongeza, “Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni mwana muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha chochote.! nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod🙏🏿#Wapo,” 

Rapper huyo hakuweka wazi ni nani anataka kufanya hivyo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.