KWANINI UPWEKE NI HATARI KWA AFYA?

Kuwa mpweke kwaweza kuwa hatari kwa afya mara mbili zaidi ya hatari itakanayo na kuwa na uzito mkubwa, kutokana na utafiti uliofanyika, mtu anapohisi kutengwa, au kutengwa na jamii yake inakuwa hatari sana husani mtu huyo anapokuwa amefikisha umri wa kati.
Utafiti uliofanyiwa kwa watu walio na umri zaidi ya miaka 50 umegundua kuwa watu waliokuwa wapweke walikuwa katika hatari ya kufa mapema mara mbili zaidi ya wale waliokuwa wamezungukwa na jamii zao, 
matokeo hayo yalionekana baada ya miaka mingi ya utafiti huo.

Katika utafiti huo, ulinganisho wa wastani wa idadi ya watu waliofanyiwa utafiti, wale waliosema walikuwa wapweke walikuwa na asilimia 14 ya hatari ya kufa mapema. Kiwango hicho ni mara mbili ya hatari itokanayo na kuwa na uzito mkubwa kati ya hao waliofanyiwa utafiti.

Utafiti uliofanyika kwa wale walio wazee huko Uingereza katika mwaka wa 2012 wanasayansi waligundua kuwa, wazee wengi walijihisi wapweke na waliotengwa muda wote, na hali hiyo ya kutengwa iliongezeka zaidi wakati wa mwisho wa wiki(weekend) na nyakati za usiku.

Tafiti nyingi zilizofanyika zimeonyesha kuwa, upweke unahusiana moja kwa moja na magonjwa kama shinikizo la damu, udhaifu wa kinga ya mwili, hatari kubwa ya kupata msongo wa mawazo, shambulizi la moyo na kiharusi.

“Watu huwa na mtazamo usio wa kawaida kuhusu kustaafu kazi. Wengi hufikiri kustaafu ni kutengana na marafiki, familia na watu wengine na kutafuta sehemu tulivu za kumalizia maisha kwa furaha. Lakini inawezekana hilo sio jambo zuri “ mwandishi wakitabu cha upweke (Loneliness)John Cacioppo alisema.

Watu ambao wataendelea kuwa karibu na wafanyakazi wenzao,familia zao, marafiki na ndugu wengine baada ya kustaafu wanazidi kuwa wachangamfu na wasio na upweke. Kuwa na muda wa kufurahia maisha na tumia nyakati za furaha na familia na marafiki. Watu wasio wapweke ni wale walio karibu na familia, marafiki na jamaa.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.