SERIKALI YAWATAKA WAAJIRI KUJISAJILI KWENYE MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano WCF, Laura Kunenge akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama katika banda la WCF wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi mwaka 2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
*****
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagamaametoa wito kwa waajiri wote nchini kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) kama sheria inavyotaka.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali pa kazi duniani yaliyofanyika Aprili 28,2017 kitaifa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro, alisema bado kuna mwamko mdogo kwa waajiri kujisajili katika Mfuko huo.
“Serikali inathamini sana juhudi zenu kama waajiri katika kuajiri wafanyakazi, niwaombe sana Chama Cha Waajiri nchini tushirikiane katika kuongeza hamasa ya kujisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ili hatimaye, Wafanyakazi wenu waweze kupata stahiki (Mafao), zao pindi wapatwapo na matatizo ya kiafya wanapokuwa kazini,” alisema Waziri Mhagama.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary alisema mpaka sasa kati ya waajiri 23,000 waliowabaini ,waajiri 6,700 pekee ndiyo wamesajiliwa katika mfuko huo hivyo kuiomba serikali isaide kuhamasisha waajiri wajisajili kwenye mfuko huo.
Katika hatua nyingine Dkt. Omary alisema katika kipindi cha Mwezi Julai,2016 mpaka Machi 31,2017 wamepokea taarifa ya matukio 478 kutoka kwenye maeneo ya kazi.
Dkt. Omary alisema kati matukio hayo 478,matukio ya ajali ni 454,magonjwa sita na vifo 18 katika maeneo ya viwandani,migodini na vyombo vya usafiri ambapo waliopata ajali huduma ya fao la matibabu.
Aidha alisema mfuko huo unatoa mafao 7 ambayo ni mafao ya huduma ya matibabu,malipo ya ulemavu wa muda,malipo ya ulemavu wa kudumu,malipo ya anayemhudumia mgonjwa,huduma za ukarabati na ushauri nasaha,huduma za mazishi na malipo ya wategemezi.
Angalia picha za matukio yaliyojiri katika banda la WCF katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.Mh. Jenista Mhagama (aliyevaa nguo nyeupe) akisalimiana kwa kushikana mkono na Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF Zaria Mmanga alipotembelea banda la WCF wakati wa maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi mwaka 2017 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano WCF, Laura Kunenge akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mh.Jenista Mhagama katika banda la WCF
Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary akiwasilisha mada fupi kuhusu Mfuko huo ambapo alisema walengwa wa mafao yanayotolewa na WCF kuwa ni wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi ambao wataumia au kuugua kutokana na kazi walizoajiriwa nazo.
Dkt. Abdulssalaam Omary aliongeza kuwa walengwa wengine wa Mfuko huo ni wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kutokana na ajali au ugonjwa uliotokana na kazi. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama akisikiliza mada fupi katika banda la WCF.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary kuhusu mwitikio wa waajiri kujisajili katika Mfuko huo ambapo Dkt. Omary alisema bado mwikitio hauridhishi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,(WCF), Dkt. Abdulssalaam Omary.Katikati ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Hadija Mwenda
Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu na Tathmini kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF, Dkt. Abdulssalaam Omary akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la WCF kuhusu mfuko huo ambao ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya fidia kwa wafanyakazi (sura 263 marejeo ya mwaka 2015).
Kulia ni Afisa Rasilimali Watu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi – WCF,Lilian Msaki akitoa elimu kuhusu Mfuko huo kwa wananchi waliotembelea banda la WCF.Alisema lengo la kuanzishwa mfuko huo ni kushughulikia masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia,kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF, Bi.Zaria Mmanga, (kulia), akielezea kuhusu Fao la huduma ya matibabu ambapo alisema pale mwajiriwa anapoumia au kuugua atapatiwa matibabu na huduma mbalimbali ikiwemo kupatiwa viungo bandia, malipo ya dawa, kumuona daktari, huduma za upasuaji, uuguzi na kurudia matibabu pale inapobidi.
Kulia ni Mwananchi akiuliza swali kuhusu Fao la Malipo ya Ulemavu wa muda mfupi na ulemavu wa kudumu kwa Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Zaria Mmanga
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi.Zaria Mmanga, (kulia), akielezea kuhusu msaada wa mazishi unaotolewa kwa familia ya mfanyakazi endapo mfanyakazi atafariki kutokana na ajali au ugonjwa uliotokana na kazi pamoja malipo yanayotolewa kwa wategemezi wa marehemu.
Afisa Fedha Mwandamizi kutoka Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw.Vicent Stephen akitoa elimu kwa wananchi juu ya malipo kwa anayehudumia mfanyakazi aliyepata ajali au kuugua kutokana na kazi na ambaye hawezi kujihudumia
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF, Bi. Zaria Mmanga akielezea kauli mbiu ya CWF kuwa ni "Fidia Stahiki kwa wakati na maendeleo ya taifa letu" na mawasiliano zaidi namba za kupiga simu bure WCF ni 0800110028 au 0800110029
Afisa Utawala Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi - WCF,Ally Shekha akionesha picha za wafanyakazi walioumia kazini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi