SAKATA LA BOS WA UN ALOFUKUZWA LIMETUA BUNGENI

 Bosi wa UN kufukuzwa latua bungeni



Dodoma. Sakata la kufukuzwa nchini la bosi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Awa Dabo, limetua bungeni.

Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga(Chadema) akizungumza bungeni leo,  aliitaka serikali kufafanua sababu za kumfukuza nchini Mkurugenzi Mkazi huyo wa UNDP Tanzania kwa kumpa saa 24.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliliambia bunge kuwa serikali ina mamlaka yote katika masuala ya kidiplomasia na hivyo bunge haliwezi kuhoji  sababu za mkurugenzi huyo kufukuzwa.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.